Lulu akiwa anaingia Mahakamani leo january 28 2013 akiwa na shauku ya kupata dhamana.
Upande wa familia ya Lulu umesema masharti yote yaliyotajwa wanaweza kuyatimiza leo leo hivyo wanasubiri tu jibu la msajili ambae ndio anatakiwa kuhakikisha hayo masharti yametimia kisha ruhusa ya kumkabidhi Lulu kwa familia yake itolewe.
Taarifa za ndani ni kwamba uwezekano wa Lulu kuachiwa upo kuanzia january 29 2013 ambayo ni kesho kwa sababu kuna watumishi wawili wa serikali ambao wapo kikazi mkoani Pwani na ndio walitakiwa kutia saini dhamana ya Lulu wakiwa ni sehemu ya masharti.
.
.
.
.
Hapa
ni wakati alipocheka sana pale mwandishi mmoja wa kike ambae pia alikua
akimpiga picha alipokua akimlainisha Lulu kwa maneno baada ya mwigizaji
huyo kuficha uso wake alipokua akipigwa picha, alisema alikua anaumizwa
macho na mwanga wa kamera.
.
.
Mama mzazi wa Lulu ni mwenye nguo nyeupe na nyeusi.(PICHA ZOTE NA MILLARD AYO.COM)
No comments:
Post a Comment