Meneja Mkuu wa Kampuni ya Green Waste Pro, Elizabeth Scheepers akishiriki kufanya usafi |
Usafi ukiendelea kufanyika katika eneo hilo |
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilaala Jerry Silaa (kulia), alikuwa ni miongoni mwa viongozi waliojitokeza kufanya usafi baada ya kuzinduliwa kwa kampeni hiyo. |
Lundo la vifuu vya madafu vikiwa kando ya ufukwe wa Bahari ya Hindi katika eneo hilo na kuharibu kabisa mandhari ya ufukwe huo, vifuu hivyo viliondolewa katika kampeni hiyo. |
Joshua Palfreman ambaye alijitolea
kufanya usafi katika uzinduzi wa kampeni hiyo akiokota takataka katika
uzinduzi wa kampeni hiyo.
Na Dotto Mwaibale
MEYA wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa
leo amezindua kampeni ya usafi katika jiji la Dar es Salaam hasa maeneo
ya Kati kati ya jiji.
Kampeni hizo zimefunguliwa na Meya huyo
na kuhudhuriwa na wadau wengine mbalimbali kutoka sekta binafsi,
wananchi na viongozi wa kampuni ya Green Waste pro.
Silaa alitoa mwito kwa wakazi wa
Manispaa ya Ilala kujenga tabia ya kushiriki katika usafi wa jiji
kuanzia kwenye kata na kuwa uzinduzi wa leo umehusisha Kata tatu ambazo
ni Kata ya Kivukoni, Mchafukoge pamoja na Kata ya Kisutu.
"Kwa kuanzia tumeanza na kata hizi
katika Manispaa ya Ilala lakini baadae zitahusishwa na Manispaa
nyingine ili kuliweka jiji katika hali ya usafi.
Uzinduzi wa kampeni hiyo ulienda
sambamba na utoaji wa elimu ambayo itafanyika katika mashule mbalimbali
na Taasisi nyingine ikiwa na lengo la kuhamasisha wananchi kuwa na tabia
ya kujali elimu ya mazingira na maeneo yanayo wahusu.
No comments:
Post a Comment