Thursday, December 20, 2012

JIWE LA MSINGI LA UJENZI WA BARABARA YA MBEYA -CHUNYA-MAKOLONGOSI LILILOWEKWA MWAKA 2008 NA RAIS JAKAYA KIKWETE LIMENG'OLEWA

Jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya Mbeya-Chunya-Makolongosi lililowekwa mwaka 2008  na Rais Jakaya Kikwete limeng’olewa. huku pamebaki alama ya X 
Wakazi wengi wa mbeya wameshindwa kuelewa kuwa jiwe wameweka serikali na ndiyo hao hao wanaweka x inamaan hapo hapastahili kuka jiwe hilo? au ndiyo baraba hiyo ya chunya haijengwi tena ?

Barabara ya Mbeya – Lwanjilo yenye urefu wa kilomita 36 ambayo ni sehemu ya barabara kuu ya
Mbeya – Chunya hadi Makongolosi yenye urefu wa kilometa 115
inayounganisha mkoa wa Mbeya na mikoa jirani ya Tabora na
Singida. Barabara hii ni kiungo muhimu kwa mikoa ya Nyanda za
juu kusini magharibi na kanda ya Ziwa. jiwe la msingi la ujenzi wa barabara hiyo liliwekwa na Rais Jakaya kikwete oktoba 2008 cha kushangaza sasa jiwe hilo limepigwa  alama ya X 
Barabara hii mpaka sasa inazidi kuharibika
Picha na Mbeya yetu

No comments:

Post a Comment