Wednesday, November 14, 2012

TCRA YADHAMINI WANAFUNZI 9 WA ELIMU YA JUU, YAAHIDI KUWASOMESHA TEHAMA

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano, Tanzania TCRA Prf John Nkoma akizungumza katika  Hafla ya kutoa Udhamini wa kuwasomesha wanafunzi wa Elimu ya Juu masomo ya TEHAMA, ambapo alisema kuwa mwaka huu wanatumia kiasi cha shilingi milioni 132 kuwasomesha wanafunzi hao pamoja na mahitaji mengine.
 TCRA imetoa udhamini kwa wanafunzi tisa wakiwemo wasichana wanne na wanaume watano ambapo jambo hili lilikuwa ni mwendelezo baada ya mwaka jana kutoa udhamini kwa wanafunzi 8.

Wanafunzi hao watasomeshwa katika vyuo vya hapahapa nchini Tanzania ambapo kwa wale wanafunzi wenye mikopo ya TCU itasitishwa na mikopo hiyio ya TCU itaenda kuwasaidia wanafunzi wengine, kwani TCRA tayari  imewasiliana na (TCU) Bodi ya Mikopo ya Vyuo vikuu kuhakikisha kuwa wale wanaodhamini wa na TCRA wenye mikopo TCU inasitishwa ili wabaki na udhamini mmoja tu ambao ni TCRA. Hafla hiyo imefanyika jana katika Makao makuu ya TCRA jijini Dar es Salaam.
Mgeni Rasmi katika Hafla hiyo ambaye ni Katibu Mkuu wa wa Wizara ya Mawasiliano sayansi na Technologia Dk Florence Turuka akiishukuru TCRA kwa uamuzi iliyochukuwa na kusema kuwa anaimani kuwa Elimu ya Tanzania itakuwa kwa kiwango cha juu.

Katibu mkuu akimkabidhi cheti maalum mdhaminiwa  ambaye ni mwanafunzi wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam ambapo cheti hicho ni ishara ya Udhamini wa TCRA.

Cheti chenyewe ndo hichi hapa

Mwanafunzi wa UDSM  Master akipokea Cheti

Baadhi ya Wadhaminiwa wakiwa na wazazi wao

No comments:

Post a Comment