Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali na kumpa pole Katibu wa Mufti wa
Zanzibar Sheikh Fadhili Suleiman Soraga ambaye amelazwa katika chumba
cha dharura katika Hospitali ya Taifa ya Muhiombili kufuatia majeraha ya
usoni na kifuani yaliyotokana na kurushiwa Tindikali na watu
wasiojulikana wakati akifanya mazoezi katika Kiwanja cha Mwanakwerekwe
mjini Unguja juzi. Rais ambaye amerejea leo Jumanne Novemba 6, 2012
akitokea katika ziara ya kikazi ya takriban juma moja katika mikoa ya
Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Singida, amemtakia Sheikh Soraga nafuu
ya haraka |