Friday, November 2, 2012

NAIBU WAZIRI WA FEDHA AITAKA RESOLUTION INSUARANCE KUAJIRI WATANZANIA

Naibu waziri wa Fedha Mh, Janet Mbene akizungumza katika  Uzinduzi wa  Kampuni ya Bima ya Resolution nchini Tanzania ambapo ameitaka kampuni hiyo kuhakikisha kuwa inawaajiri watanzania na kulipa kodi jambo ambalo litasaidia kupunguza umasikini  Nchini.
Amesema kuwa  anawataka watanzania kujiunga katika  mfuko huo wa bima ambao haubagui mzee au kijana na pia upo katika nchi zote za Afrika Mashariki.

Oscer Osir  Meneja wa Kampuni ya Resolution  Tazania akizungumza katika uzinduzi huo ambapo alisema kuwa  anawataka watanzania kujiunga katika mfuko huo ili wafaidike kutokana na Resolution. Na ameongeza kuwa wanaimani kwamba uchumi wa Tanznia Utakua kutokana na Mfuko huo wa Bima.

Naibu waziri akiwa kwenye Picha ya pamoja na uongozi mzima wa Resolution innsuarance

Baada ya uzinduzi watu walipandisha glasi zao zilizokuwa na vinywaji kuashiria shangwe