Viongozi wa jumuiya Uamsho Kisiwani Zanzibar Umeipa Serikali ya Zanzibar Saa 26 ihakikishe kuwa Kiongozi wao ambaye ni Sheikh Farid amepatikana.
Akizungumza katika mkutano na waislamu leo Kisiwani humo Kiongozi wa Kikundi cha Uamsho Sheikh Amir Azzan amesema kuwa wanatoa Muda wa saa 26 mpaka kesho sa 10 alasir Serikali ihakikishe kuwa sheikh Amir Farid awe ameachiwa.
Sheikh Amir, amewataka waislamu wawe na subira na watunze Amani hadi kesho baada ya Muda walioutoa ambapo amesema kuwa endapo hatapatikana ndani ya ,Masaa hayo watatoa Tamko lao.
Amesema kuwa ccm, Jeshi la polisi na Jeshi la wananchi Tanzania wamehusika Kumteka Sheikh Farid kwa habari waliozipata.
Inasemekana walomteka walikuwemo wanajeshi wawili na polisi wa ffu 2 na viongozi wa ccm.
"Tunaiman Amir Farid bado yuhai na yupo hapa hapa Zanzibar.
Safari hii mpaka kieleweke" amesema Sheikh Amir.