Wednesday, October 31, 2012

MTU AMBAKA MWANAMKE HADHARANI

Mtu mmoja anayetajwa kuwa ni Mwanajeshi  amembaka mwanamke  hadharani eneo la Magomeni Makanya Jijini Dar es Salaam mchana huu kwenye mida ya saa 6.

Kwa simulizi ya shuhuda aliyekuwepo kwenye eneo la tukio hilo, ambaye pia anamfahamu huyo mjeshi mpaka nyumbani kwake kasema kuwa jamaa kakutana na huyo mwanamke karibu na gereji bubu ya barabarani makanya, mara akamshika kwa nguvu huyo mwanamke na kumvua kwa nguvu hadhari na kumtenda hicho kitendo cha aibu mbele ya macho ya watu wengi waliokuwa wakipita hapo. Mpaka anamaliza kitendo hicho, kulikuwa na watu wengi waliofurika hapo wakiwa wameduwaa. Kwa nini hawakumpiga? Ni jamaa wanayemfahamu (kwamba ni mjeshi, pia ni mbabe), na anaishi maeneo ya karibu (Mwananyamala Kisiwani-ambapo si mbali na gereji hiyo).


Shuhuda mmoja aliyetaka kumtetea huyo dada alijikuta akionja hasira ya huyo mjeshi. Jamaa kamvunjia vioo vya gari yake kwa hasira; kisha akasogea karibu kucheza mchezo wa pool.


Muda mfupi; walifika askari polisi na difenda yao-wakiwa na bunduki zao. Huenda walipigiwa simu na wananchi. Polisi hao wameshindwa kumkamata mjeshi huyo; ambaye walikuwa wanamuona na yeye wala hakuwakimbia.


Binafsi nimefika eneo hilo la tukio takriban nusu saa baada ya tukio na kuukuta huo umati wa watu, polisi wakiwepo na difenda lao. Kama vile haitoshi, mjeshi huyo kawazonga polisi na kuwaambia kuwa hawana UBAVU wa kumkamata wala nini. Ndiyo hayo yaliyotokea muda mfupi uliopita.


Kwa mujibu wa mtoa taarifa wa habari hizi alipopigiwa simu alisema kuwa alifika eneo hilo na alimkuta mtu huyo akiwa amezingirwa na watu, ameweka namba yake ya simu katika mtandao 0764600170


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Charles Kenyela alipoulizwa kuhusiana na Tukio hili alisema kuwa, yeye hakuwa na taarifa na kwamba labda habari hizo zipo lakini bado hajaletewa taarifa ofisini kwake.

"Kiukweli leo siku nzima nlikuwa  nimeshinda kwenye kikao hivyo bado sijaweza kujua yaliyotokea siku ya leo hivyo ndugu mwandishi naomba tuwasiliane kesho nitakupa taarifa sahihi", alisema Kenyela.