Msanii Kalapina wa kikosi cha mizinga ameamua kuweka wazi kwa nini anaona serikali inafanya masihara kwenye sekta ya Afya.
Namkariri
akisema “juzi nilikua Muhimbili nasumbuliwa na vidonda vya tumbo kuna
kipimo kinaitwa OGD cha kupima mfumo mzima wa chakula, kile kipimo
Muhimbili hakipo na wakati kipo kinafanya kazi gharama ilikua laki moja,
ni pesa nyingi sana kwa mlalahoi kumudu”
“hawa
madaktari wanapogoma wanahaki ya kugoma kutokana na hakuna vitendeakazi
watanzania wanakufa, sekta ya afya ni sekta muhimu sana wabongo
wanapiga kelele tu serikali inakusanya mapato mengi wawekezaji
wamewekeza kwenye migodi, kwenye kila sekta lakini tunashindwa kuelewa
serikali inashindwa nini kuboresha huduma za afya, inakusanya kodi hizi
pesa zinakwenda wapi? huduma ya afya inabidi itolewe bure”
kwenye
line nyingine kuhusu Dr Ulimboka, Kala amesema ni mpiganaji, hamshauri
kabisa aondoke nchi hii kwa sababu mchango wake na taaluma yake
inahitajika, haya madaktari walio nje ya Tanzania warudi nyumbani.
---
Habari via MillardAyo.com