MKURUGENZI wa Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma
(PSPF), Patrick Mongella, amesimamishwa kazi kuanzia Oktoba 15 mwaka
huu, kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili.
Chanzo cha kuaminika kutoka PSPF kimesema kwamba, kusimamishwa kwa
mkurugenzi huyo, kumetokana na agizo la Bodi ya Wadhamini ya PSPF, baada
ya kubaini kuwapo namna ya kutotekeleza majukumu yake ipasavyo, pamoja
na kutotii maagizo halali ya wakubwa wake kuhusiana na uendeshaji wa
shughuli za mfuko.
Pia, habari za ndani zinaeleza kuwa kiongozi huyo hakuwa na mahusiano
mazuri ya kikazi na watumishi wenzake wa mfuko wa kada zote, akidaiwa
kuwa ni mwenye dharau, kiburi, majivuno na lugha chafu kwa watumishi
walioko chini yake, wakiwamo viongozi wake wakuu.
Chanzo hicho kimefichua kwamba, majigambo ya bosi huyo yanatokana na
yeye kujivunia jina la mama yake, ambaye aliwahi ni mkongwe katika
nyanja mbalimbali za siasa ndani na nje ya nchi na ukaribu aliokuwa nao
na baadhi ya viongozi waandamizi wa serikali hapa nchini.
Taarifa zaidi zinapasha kuwa, kiongozi huyo aliyepewa dhamana ya
kuongoza kurugenzi nyeti katika taasisi hiyo muhimu, hakuwa na sifa na
vigezo hitajika vya kitaaluma wakati wa ajira yake, hivyo kupelekea
kusaka sifa hizo baada ya kupewa nafasi hiyo.
Watumishi wengi wa PSPF wamepokea agizo hilo la bodi kwa furaha kubwa,
maana kiongozi huyo alikuwa ni kero na kikwazo kikubwa tena cha muda
mrefu sana, husus
|