Friday, October 19, 2012

ASKARI MWINGINE AUAWA ZANZIBAR

Vurugu huko Zanzibar zinazidi kuchukua Sra mpa baada ya leo taarifa kutufikia kuwa  usiku wa kuamkia leo kuna askari mwingine ameuawa na watu wanaosadikiwa kuwa ni kikundi cha Uamsho wanaomtafuta kiongozi wao aliyepotea katika mazingira ya kutatanisha Sheikh Farid.

Habari hizo zinasema kuwa  safari hii askari aliyeuawa  ni askari wa kike ambaye inasemekana nae ameshambuliwa na wanaodhaniwa kuwa ni wafuasi wa kikundi cha UAMSHO.

Huu utakuwa ni muendelezo wa mauaji ya askari huko Zanzibar baada ya jana kuriporiwa kuuawa kwa koplo Said Abdulrahman...