Monday, February 11, 2013

SERIKALI YASHAURIWA KUTUMIA LUGHA YA KENGEREZA KATIKA SHULE ZA MSINGI


Mkurugenzi wa Taasisi ya VEPK Bi, Ketty Allen, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam wakati wa Uzinduzi wa kitabu cha kumwongoza mwalimu kufundisha Kingereza.
 
Serikali imeshauriwa kupitisha Mtaala wa  kutumia lugha ya kingereza katika kufundishia shule za msingi ili kuwasaidia wanafunzi kuielewa lugha hiyo pindi wanapokwenda katika elimu ya sekondari na elimu za juu.



Hayo yamesemwa na Mratibu wa Taasisi ya Elimu ya mpango wa elimu vijijini VEPK (village education project Kilimanjaro) Bw Dilly Mtui  leo jijini dar es salaam wakati alipokuwa akizindua kitabu kipya cha mwongozo kwa waalimu wa shule za msingi kitakacho wasaidia walimu kufundisha kwa ufasaha kiingereza katika shule za msingi.



Bw Mtui amesema moja ya sababu ya wanafunzi kufeli sana katika elimu ya sekondari ni maandalizi mabovu wanayoyapata wakati wakiwa shule za msingi,amesema katika shule za msingi wanafunzi hujifunza kwa Kiswahili jambo linalowawia gumu wakati wanapoingia sekongari na kukuta masomo kwa lugha ya kiingereza.

Ameongeza kuwa  serikali inapaswa kuwasaidia walimu wa shule za msingi ikiwa ni pamoja na kuwapelekea vitabu vya kutosha na miundo mbinu mizuri ya kufundishia ili waweze kufikisha elimu bora kwa wanafunzi wao.

Kwa upande wake  Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Bi, Katty Allen MBE amesema kuwa sio tu wanatoa vitabu kwa ajili ya walimu ila bado wana vitabu vya  wanafunzi vya kuanzia Darasa la Kwanza na kuendelea.









Baadhi ya waaandishi wa habari waliokuwemo katika mkutano huo


Mratibu wa Taasisi hiyo akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari

Moja ya Kitabu kinachozalishwa na Mradi huo


No comments:

Post a Comment