Saturday, January 26, 2013

MAGEREZA WA PWANI SASA KULA RAHA

Kamishna wa Magereza Nchini John Minja akizungumza katika Uzinduzi wa Mabasi ya kusafirishi Magereza Mkoani Pwani ambapo amewataka wahusika kuyatumia Mabasi hayo kwa uaminifu. Uzinduzi huo umefanyika leo katika katika gereza la Mifugo Ubena eneo la Bwawani mkoani Pwani kwa ajili ya kuzindua mradi wa kusafirisha mahabusu kutoka gerezani kwenda mahakamani kwa mkoa wa Pwani.

Baadhi ya Magari ya kusafirishia Mahabusu kutoka Gerezani kupelekwa mahakamani yaliyozinduliwa leo Mkoani Pwani ambapo yamezinduliwa Magari kumi mkoani humo.

Naibu waziri Silima akikata utepe kuashiria uzinduzi wa magari hayo

Naibu waziri Perera Ame Silima  ambaye ni Naibu waziri wa Mambo ya Ndani akijaribu kuendesha Moja ya Basi litkalotumika kusafirishia Abiria

No comments:

Post a Comment