Thursday, September 6, 2012

NAIBU WAZIRI MKUU WA CHINA ATEMBELEA TAZARA, ASEMA ATAHAKIKISHA TAZARA INARUDIA KATIKA HALI YAKE YA ZAMANI

Balozi wa China nchini Tanzania Bw, Lu You Qing (kushoto) akisalimiana na Naibu Waziri mkuu wa China  Hai Liang Yu, mara baada ya kuwasili katika makao makuu ya Reli ya Tazara leo hasubui. 
Leo naibu waziri mkuu wa China Bw, Hai Liang Yu, ametembelea  Reli TAZARA ambapo amesema kuwa watahakikisha TAZARA inaboreshwa na kurudia katika hali yake ya zamani kama walivyoiacha kipindi cha nyuma.Ujio wake pia TAZARA utarekebisha mashine za kutengeneza magari zilizopo Katika Reli ya TAZARA na pia kuhakikisha kuwa Reli ya TAZARA inafanya vizuri katika Safari zake.


Naibu Waziri mkuu wa China Bw, Hai Liang Yu, akisalimiana na Mmoja wa maafisa wa Tazara mara baada ya kuwasili TAZARA leo.

Naibu Waziri mkuu wa China Bw, Hai Liang Yu, akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Uchukuzi nchini Tanzania Harisson  Mwakyembe wapili kulia walipotembelea makao makuu ya Reli ya Tazara leo hasubui.

TAZARA leo hasubui palikuwa hivi

Balozi wa China nchini Tanzania Bw, Lu You Qing (kushoto) akimuelekeza Naibu waziri wa China Hai Liang Yu wapili kutoka kulia pamoja na maafisa wengine namna TAZARA inavyofanya kazi.