Monday, September 10, 2012

HIZI PICHA NI ZA WAKAZI WALIOVUNJIWA PAMOJA NA KUCHOMEWA NYUMBA ZAO KWA MADAI YA KUWA NI WAVAMIZI KATIKA MTAA WA MADALE WILAYA YA KINONDONI, WAKAZI HAO WAPO ZAIDI YA 4000 NA KWAMBA WOTE HAO HAWAJAHESABIWA KWA KILE WANACHODAI KUWA HAWANA MAKAZI

Huyu anaonyesha Maganda ya Risasi yaliyokuwa yanatumika wakati wanafukuzwa katika maeneo hayo

Baada ya kuchomewa nyumba yake dada huyu analala hapa yeye pamoja na watoto wake wawili ni nje ya shule mpya inayojengwa huko madale

Naye huyu yupo kwake anapika


Hapa pia ni kambi ya mtu mwingine na familia yake


Huyu ndo mwenye nyumba hii ana watoto wawili na mke na wote wanaishi humu ndani




Hii ndiyo shule


Wakazi hao wanaiomba serikali iwape makazi ya kuishi kwani wanateseka kukaa bila makazi hivi sasa.