- Jaji Mstaafu Stephen Iihema - Mwenyekiti na Kiongozi wa Tume hii
- Theophil Makunga (Tanzania Editors Forum (TEF))
- Pili Mtambalike (Media Council of Tanzania (MCT))
- Kanali Wema Wapo (JWTZ)
- Isaya Mangulu, Mtaalamu wa Mabomu ambaye ni Naibu Kamishina
Tume hiyo imetakiwa, ndani ya siku 30, kupata taarifa zenye majawabu ya maswali 6 ambayo yanawatatiza Wananchi.
Waziri akayataja maswali hayo kuwa ni:
- Kipini chanzo cha mauaji ya Mwangosi
- Kama kuna ukweli kuwa kuna uhasama kati ya polisi wa Iringa na waandishi wa habari wa mkoani humo
- Kama ni kweli kuna waandishi watatu wa mkoani Iringa ambao wako kwenye orodha ya kuuawa na polisi
- Kama nguvu iliyotumiwa na polisi Nyololo ilikuwa sahihi
- Kama kuna utaratibu kwa vyama vya siasa kukata rufaa kama haviridhiki na uamuzi wa Polisi
- Kama kuna uhusiano mbaya kati ya polisi na baadhi ya vyama vya siasa hapa nchini
Waziri amesema, iwapo tume hiyo itahitaji msaada wa kitaalamu kutoka nje ya nchi, Serikali iko tayari kuagiza wataalamu hao, ili waisaidie ili wapate majibu yenye taarifa zinazojitosheleza na kuridhisha.